JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI?
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wagalatia 5:19-21
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tuwe makini hapa, matendo ya mwili sio tuu hayo tuliyoambiwa hapo, ila ni pamoja na yanayofanana na hayo. Kuishi katika Kristo ni kuusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ni kujiepusha na maovu na kujitenga kabisa na matendo mabaya ya mwili. Basi walio katika Kristo waenende kwa Roho, wala hawatatimiza kamwe tamaa za mwili. Mwili hutamani ukishindana na Roho. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
1 Wakorintho 6:9-10
Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
Waefeso 5:5
Hivyo, tujiepushe na tamaa za mwili ili tuurithi Ufalme Wa Mungu.
Comments
Post a Comment