MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI
MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Mawazo yake si
mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo
juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na
mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu
anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na
usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu
wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya
amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho. Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye
atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.
BWANA asema hivi,
Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa, yaani ataokoka; na
wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.
Ndugu zangu,
tuangalie usiwe katika mmoja wetu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na
Mungu aliye hai; lakini tuonyane kila siku, maadamu iitwapo leo ili mmoja wetu
asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa maana tumekuwa washirika wa
Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetukwa nguvu mpaka mwisho.
ISAYA 55:8,9,6,7, YEREMIA 29:11-12, YEREMIA 33:3, MATENDO YA
MITUME 2:21, WARUMI 10:13 2 WAKORINTHO
6:2, WAEBRANIA 3:12-14.
Comments
Post a Comment