Skip to main content

Posts

JE! DANIELI ALISEMA NINI KUHUSU UFALME WA MUNGU?

JE! DANIELI ALISEMA NINI KUHUSU UFALME WA MUNGU? Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Ufalme na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni wa milele, na watu wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. Aliona katika njozi za usiku, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.     Malaika akamwambia Mariamu, usiogope, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya...
Recent posts

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Mawazo yake si mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho.   Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.     BWANA asema hivi, Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la B...

USIKUBALI KUKATISHWA TAMAA, NA WALA USIJIVUNIE KWA AKILI ZAKO.

USIKUBALI KUKATISHWA TAMAA, NA WALA USIJIVUNIE KWA AKILI ZAKO. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Usiisahau sheria ya Bwana, bali moyo wako uzishike amri zake. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Umewekewa mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; umeagizwa kumpenda Bwana, Mungu wako   na kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka na Bwana, Mungu wako apate kukubarikia .      Una hekima, usijisifu kwa sababu ya hekima yako, wala una nguvu usijisifu kwa sababu ya nguvu zako, wala ni tajiri usijisifu kwa sababu ya utajiri wako; bali ujisifu kwa sababu hii, unamfahamu BWANA, na kumjua, ya kuwa yeye ni BWANA, atendaye wema, na hukumu, na haki, na ...