USIKUBALI KUKATISHWA TAMAA, NA WALA
USIJIVUNIE KWA AKILI ZAKO.
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Usiisahau sheria
ya Bwana, bali moyo wako uzishike amri zake. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,
wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye
atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana,
ukajiepushe na uovu. Umewekewa mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;
umeagizwa kumpenda Bwana, Mungu wako na
kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu
zake, upate kuwa hai na kuongezeka na Bwana, Mungu wako apate kukubarikia .
Una hekima,
usijisifu kwa sababu ya hekima yako, wala una nguvu usijisifu kwa sababu ya
nguvu zako, wala ni tajiri usijisifu kwa sababu ya utajiri wako; bali ujisifu
kwa sababu hii, unamfahamu BWANA, na kumjua, ya kuwa yeye ni BWANA, atendaye
wema, na hukumu, na haki, na anapendezwa na mambo hayo, asema BWANA.
Yesu anasema, yeye
ndiye njia, na kweli, na uzima; mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya yeye.
Upatane nia zako na wengine. Usinie yaliyo makuu, lakini ukubali kushughulishwa
na mambo manyonge. Usiwe mtu wa kujivunia akili.
MITHALI 3:1,5-7, KUMBUKUMBU LA TORATI 30:15-16, YEREMIA 9:23-24, YOHANA 14:6, WARUMI
12:16.
Comments
Post a Comment