TAFAKARI: KUTAFAKARI
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Yoshua 1:8
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Ufunuo wa Yohana 22:18
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Warumi 10:17
Bwana asifiwe watu wa Mungu. Ili kusitawi sana, inabidi kutafakari Neno la Mungu mchana na usiku, bila kubadili chochote kwa kuongeza au kupunguza. Na ili ukue kiimani ni kulisikia neno la Mungu. Hivyo unaposoma Neno la Mungu mahali popote au unaposikia kwa mtu yoyote, SIKILIZA NA TAFAKARI nini Mungu anasema na wewe kupitia hilo neno.
Mbarikiwe sana na muwe na siku njema.
Comments
Post a Comment