TAFAKARI: MAFUNDISHO YA WANADAMU
Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
Msishike, msionje, msiguse;
(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Wakolosai 2:20-23
Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.
Wakolosai 2:6,9,10
Comments
Post a Comment