TAFAKARI: SIO UAMINIFU
Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Mwanzo 3:21,22,24
Bwana asifiwe watu wa Mungu. Upendo, uvumilivu na kusamehe, vyote hivyo sio uaminifu. Unaweza kupendwa, kuvumiliwa na kusamehewa lakini usiaminike. Ni kazi yako kufanya uaminike. Uaminifu ni kulikubali kosa, kujutia na kukiri kutolirudia hilo kosa ulilolifanya, kutolirudia kabisa na kufanya kila namna usifanye makosa mengine tena tofauti na hilo.
Tunaona Mungu hapa bado aliwapenda watu wake pamoja na kosa lao, akawafanyia mavazi ya ngozi akawavika. Ila kwa sababu ya matunda ya mti wa uzima, akuwaamini, akawafukuza pale bustanini. Wapendwa tuwe waaminifu kwa Mungu na kwa wenzetu pia, ili kuvumiliana, kusameheana na kupendana kwetu kudumu. Amina.
Comments
Post a Comment