TAFAKARI: MAJARIBUNI
Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
Mathayo 4:3
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
1 Wathesalonike 3:5
Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
Yakobo 1:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
1 Wakorintho 10:13
Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
Mathayo 4:1
Bwana asifiwe watu wa Mungu. Wapendwa, Mungu hajaribu wala hajaribiwi ila hutuongoza kwenye majaribu ili kutuimarisha kiimani. Anayetujaribu ni yule muovu.
Mbarikiwe sana, Amina.
Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
ReplyDeleteMathayo 4:1
Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.
Luka 4:13