ENENDA KAMA YEYE ALIVYOENENDA.
Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
1 Yohana 2:6
Amani na Upendo wa Mungu uwe pamoja nanyi.
Kwa Mkristo kuwa mkamilifu, inampasa kuishi namna Kristo alivyoishi. Kikubwa ni Upendo maana ndio kifungo cha ukamilifu na ndiyo amri mpya aliyotupa, tupendane. Upendo utakuweka mbali na dhambi, na kuwa mkamilifu katika Kristo.
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Wakolosai 3:14
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Yohana 13:34
Hivyo basi tuwe na Upendo kama Kristo alivyotupenda na tuwatendee wengine mema kama yeye alivyotutendea.
Comments
Post a Comment