JE, NI AHADI GANI ALIYOPEWA MSHINDI?
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
Ufunuo wa Yohana 21:4,6,7
Neema na rehema za Mungu zowe pamoja nanyi. Kwa makwazo na mateso mbalimbali utakayokutana nayo hapa ulimwenguni, usiogope, kuwa na saburi maana kuna ahadi uliyopewa na Mungu utakapoweza kuyashinda yote. Utakuwa mwana na utarithi vyote, na wala hakutakuwa kwako na taabu tena.
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Warumi 12:21
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
1 Yohana 5:4-5
Hivyo, mshindi ni yule atakayeweza kuushinda ulimwengu ni kwa imani, na kwa kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwa kukabiliana na maovu kwa wema.
Comments
Post a Comment