KWA NINI KUOMBA NA KUSHUKURU?
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Wafilipi 4:6
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema na faraja.
Kuomba na kushukuru, ni kuonyesha uaminifu na ni mapenzi ya Mungu kwetu katika Kristo. Tukeshe tukiomba anamaanisha tusichoke kuomba, ila tuu tusiache kushukuru. Kuomba na kushukuru ndicho kinachokuweka karibu na Bwana, maana kushukuru kunaonyesha UAMINIFU.
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
Wakolosai 4:2
Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
Zaburi 145:18
Hivyo basi, tusijisumbue kwa neno lolote bali tudumu katika kusali na kuomba, bila kusahau kushukuru, maana Bwana yu karibu tukimwita kwa UAMINIFU.
Comments
Post a Comment