MAISHA BINAFSI YA IBADA.
Tunahitaji sana kuwa na maisha binafsi ya ibada, ili kuwa karibu zaidi na Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Maisha binafsi ya ibada yanahitaji mambo makuu matatu:
1. Muda wa utulivu.
2. Mahali tulivu.
3. Moyo wa utulivu.
Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana,
Mwanzo 19:27
Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
Mwanzo 28:18
Nawe uwe tayari asubuhi, na asubuhi ukwee juu katika mlima wa Sinai, nawe hudhurisha nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima.
Kutoka 34:2
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. [YESU]
Marko 1:35
Hivyo ni muhimu sana kuwa na maisha binafsi ya ibada ile uweze kufanikiwa kuwa karibu zaidi na Mungu.
Comments
Post a Comment