NI JINSI GANI PETRO ALITHIBITISHA MAHUBIRI YAKE YA UJIO WA KRISTO?
Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
2 Petro 1:16
Neema na rehema za Mungu ziwe pamoja nanyi. Petro hapa anatuthibishia kwamba maneno haya ya kinabii sio kwamba ameyasikia kwa mtu bali alikuwa na Bwana wetu Yesu Kristo, aliona ukuu wake na alisikia sauti kutoka mbinguni kwa Mungu baba ikisema " huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyeridhishwa naye" walipokuwa naye.
Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
2 Petro 1:18-20
Hivyo, unabii katika maandiko haujafasiri apendavyo mtu, wala haukuletwa kwa mapenzi ya mwanadamu, ulinenwa yaliyotoka kwa Mungu, kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Comments
Post a Comment