NI MAMBO GANI YATAKAYOJITOKEZA ZAIDI NYAKATI ZA MWISHO?
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
2 Timotheo 3:1-5
Upendo, Neema, Rehema na Amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu ziwe pamoja nanyi. Nyakati za mwisho ni nyakati hatari sana sababu watu watakosa upendo, na hatutapendana sisi kwa sisi. Bali watu watapenda na kuthamini zaidi mali na fedha kuliko utu na utii. Watu watapenda starehe kuliko Mungu tena mbaya zaidi wakijifanya watakatifu.
Na sio kwamba maovu yatapungua, yatazidi kuongezeka.
lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
2 Timotheo 3:13
Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Luka 18:8
Hivyo, ni vizuri tuzidi kujiandaa sababu hatujui hiyo siku wala hiyo saa, na tufahamu kuishi maisha matakatifu nyakati hizi za mwisho kuna kuudhiwa.
Comments
Post a Comment