NI MUHIMU KULA KILA KILICHO HALALI PEKEE?
Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
1 Wakorintho 10:23
Bila shaka hapa Paulo anazungumzia vitu tunavyoweza kula. Anasema kwa Mkristo kwa kufahamu, akila chakula ambacho ni sadaka kwa sanamu, naye atakuwa mshiriki wa ibada hiyo. Ila asipojua akila sio shida.
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1 Wakorintho 10:27,28,31
Hivyo, shida ni pale unapojua ni chakula kwa ajili ya sadaka. Bora kutoulizauliza kwa ajili ya dhamiri.
Comments
Post a Comment