NI NANI ANAYETUPA NGUVU YA USHINDI?
Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Wakorintho 15:57
Ahimidiwe Mungu baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na baba yetu, baba wa rehema na faraja yote. Anayetupa ushindi ni Mungu kwa Kristo Yesu, kwa jinsi anavyotupenda.
Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
Warumi 8:37
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Yohana 16:33
Hivyo, tumshukuru Mungu siku zote kwa kutupa ushindi dhidi ya yule adui kwa kupitia Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tuwe na amani ndani ya Kristo, maana Kristo mwenyewe ameushinda ulimwengu.
Comments
Post a Comment