TUKESHE NA KUWA NA KIASI
Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
1 Wathesalonike 5:1-2
Neema na Rehema za Mungu ziwe pamoja nanyi. Kwa habariya ile siku hakuna haja ya kuandikiwa maana twafahamu yaja kama mwivi. Ulishapata kuwa wa nuru na mwana wa mchana wala si wa giza na usiku, ile siku haitakupata kama mwivi.
Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
1 Wathesalonike 5:4-6
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
Waefeso 5:8-9
Hivyo, ni vizuri tuzidi kujiandaa sababu hatujui hiyo siku wala hiyo saa, na tukeshe ( kuwa na maisha binafsi ya ibada ) na kuwa na kiasi.
Comments
Post a Comment