UJIO WA KRISTO UMEFANANISHWA NA WAKATI GANI?
Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Mathayo 24:37
Upendo, Neema, Rehema na Amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu ziwe pamoja nanyi. Ujio wa Kristo umelinganishwa na siku za Nuhu. Hakuna mtu aijuaye, wala malaika wala Mwana, ni Baba peke yake.
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Mathayo 24:36
Tunachotakiwa ni kujiuliza ni nini kilitokea siku zile za Nuhu, na watu walikuwa katika mazingira gani? Je, walikuwa wanafahamu? Je, walikuwa wamejiandaa?
Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Mwanzo 6:5-6
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Mathayo 24:38-39
Hivyo, tuache kujiulizauliza, mbona harudi na alisema atarudi? Bali, tujiandae maana hatujui hiyo siku wala hiyo saa.
Comments
Post a Comment