UKWELI NI KUUISHI SIO KUJIFUNZA TUU.
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.
Zaburi 119:11-12
Upendo na amani ya Mungu katika Kristo iwe pamoja nanyi. Ukweli ni kuuishi huo ukweli, sio tuu kuusikia na kujifunza katika Neno kwa kuhubiriwa habari njema.
Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
Waebrania 4:2,6
Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
1 Samweli 12:23
Hivyo, tuliishi neno sio kulisikia na kujifunza tu peke yake, tusitende dhambi.
Comments
Post a Comment