UNABII KWENYE MAANDIKO SIO TAFSIRI BINAFSI.
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Petro 1:19-21
Neema na Rehema zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu ziwe pamoja nanyi. Unabii sio kutafsiri apendavyo mtu, bali ni kunena yaliyotoka kwa Mungu. Tujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo ya maana.
Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,
2 Timotheo 2:16
Hivyo, tujiepushe na mambo yasiyo ya maana, yasiyo ya dini, maana unabii mwingi wa sasa ni wa kunena mapenzi ya wanadamu.
Comments
Post a Comment