UTULIVU NA MUNGU.
Muda wako binafsi wa utulivu na Mungu, kunaongeza mahusiano na Mungu na ndio chanzo cha nguvu. Mfano wa muda binafsi na Mungu tunauona kwa Yesu mwenyewe, alikuwa akitoka na kwenda pasipo na watu kuomba.
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Marko 1:35
Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.
Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
Luka 22:39-41
Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.
Luka 5:16
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Mathayo 6:6
Comments
Post a Comment