WATASEMA NINI WALIO GIZANI KUHUSU UJIO WA BWANA?
Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
2 Petro 3:3-4
Neema na Rehema zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu ziwe pamoja nanyi. Ni jambo la kawaida sana kusikia watu wakiuliza, " alisema atarudi, mbona harudi?" Tena wakidhihaki " Nisubiri mpaka lini, mpaka Yesu arudi?" Bila kufahamu kwamba hata wakati wa gharika ilikuwa hivyo hivyo, dunia ikaangamia kwa maji, ila kwa sasa ni kwa moto. Ni upendo tuu, ndio maana anakawia.
Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
2 Petro 3:9
Hivyo, ni vizuri tuzidi kujiandaa sababu hatujui hiyo siku wala hiyo saa, maana kuja lazima aje na hukumu ipo palepale.
Comments
Post a Comment