ILI UKUE KWA NENO LA MUNGU, NI LAZIMA MTU AFANYE NINI NALO?
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Zaburi 119:11
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ni lazima Neno la Mungu liwekwe mioyoni mwetu, lihifadhiwe kabisa hapo, ili lituwezeshe kujiepusha na kutenda dhambi. Neno lenye pumzi ya Mungu lafaa sana kwa kufundisha, kuonya, kuongoza na kuadabisha katika haki.
Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.
Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako.
Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.
Zaburi 119:12,15,16
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
2 Timotheo 3:16
Hivyo, tujitahidi sana katika kuwa na muda wa utulivu, moyo wa utulivu na mahali tulivu, ili tupate wakati mzuri na Mungu wa kuzungumza naye kwa kuomba, kushukuru na kusikiliza anasema nini nasi kupitia Neno lake. Maisha ya utakatifu yanahitaji sana MUDA WA UTULIVU NA MUNGU.
Comments
Post a Comment