JE, HUU UZIMA WA MILELE UMEFICHWA VIPI KWA MWAMINI?
Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
Wakolosai 3:3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Tuvifishe viungo vyetu vilivyo katika nchi, tuepukane na maovu sababu huleta ghadhabu ya Mungu. Yawekeni mbali maovu mkivaa utu mpya.
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
1 Yohana 5:11-12
Hivyo, mna uzima wa milele ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu, na uzima huo umefichwa pamoja naye katika Mungu.
Comments
Post a Comment