JE, KUFUNDISHANA HUKU NA KUABUDU HUKU KUNAKUBALIKA NA BWANA?
wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Isaya 30:10
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tatizo kubwa watu wamemkaribia Mungu wakimuabudu, wakimsifu na kumheshimu kwa vinywa vyao tuu, mbali mioyoni mwao ni mawazo ya kibinadamu iliyofarakana na Mungu, kwa mafundisho na maagizo ya wanadamu.
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Isaya 29:13
Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,
Marko 7:6-7
Comments
Post a Comment