JE, MAFUNDISHO YA UKAMILIFU YAMEFUNDISHWA KATIKA BIBLIA?
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Yakobo 1:4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tusiogope majaribu, maana kujaribiwa kwa imani huleta saburi, na Neno la Mungu linasemani furaha kuangukia majaribu, na kwa saburi tupate kuwa wakamilifu. Pia, upendo ndio kifungo cha ukamilifu.
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
Yakobo 1:2
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Wakolosai 3:14
Hivyo, tusiogope majaribu tukihesabu ni furaha tupu kwa saburi tupate kuwa wakamilifu, na tupendane sisi kwa sisi kama Kristo Yesu alivyotupa amri. Asiyependa hukaa katika mauti. Asiyetenda haki hatokani na Mungu, ni wa ibilisi.
Comments
Post a Comment