JE, MTU ANAWEZAJE KUKUA KATIKA NEEMA?
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Petro 1:4-8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Asiyekuwa na hayo ni kipofu haoni vitu vya mbali na amesahau kutakaswa dhambi zake za zamani, maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Tena tusichoke katika kutenda mema, kwa kadri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema.
Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
1 Yohana 2:9-10
Comments
Post a Comment