JE, NENO LA MUNGU LINAKUWA NINI MOYONI MWAKO?
Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.
Yeremia 15:16
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Usirudi nyuma na kuziacha amri zake Mungu, na yatunze maneno yake zaidi ya riziki yako. Maneno yake yakafanye kinywa chako kuwa kitamu kama asali na likiwe furaha na shangwe kwa wengine pia.
Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.
Ezekieli 3:1
Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.
Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.
Ufunuo wa Yohana 10:10-11
Comments
Post a Comment