JE! NI KWA NAMNA GANI TULIPATA UNABII KATIKA MAANDIKO?
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Petro 1:21
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Unabii katika maandiko uliwafikia wanadamu kutoka kwa Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na si kwa jinsi apendavyo mtu fulani. Neno liliwajia wengine pia kwa Bwana kusema nao katika ndoto.
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
2 Petro 1:20
Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.
Hesabu 12:6
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Hesabu-Numbers 12:8
Hivyo, unabii katika maandiko umewafikia wanadamu kwa baadhi kuongozwa na Roho Mtakatifu, wengine Bwana kusema nao katika ndoto na wengine kusema nao mdomo kwa mdomo (waziwazi).
Comments
Post a Comment