JE, NI LINI HIZO AHADI ZA THAMANI ZITAFIKIWA?
Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
Waebrania 10:36-38
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa ujasiri tulio nao, tuendelee kuwa na saburi, maana anayekuja hatakawia. Bali tuishi kwa imani bila kusitasita kuokoa roho zetu.
Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
2 Petro 3:13-14
Hivyo, tuishi kwa imani, tuonekane katika amani bila mawaa, wenye ujasiri, wenye saburi. Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
YEYE ATAKUJA, WALA HATAKAWIA.
Comments
Post a Comment