JE, NI NINI KITASABABISHA MKRISTO KUKUA?
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
1 Petro 2:2
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa Mkristo kukua ni kumwendea Kristo Yesu kwa kukaa katika Neno la Mungu siku zote. Na pia kuhakikisha unapata muda wa utulivu, moyo wa utulivu na mahali tulivu na Mungu siku zote.
Ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
1 Petro 2:1,4
Comments
Post a Comment