JE, NI WAKATI GANI SAHIHI KUOMBA MSAADA KWA MUNGU?
Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Wafilipi 4:6
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wakati wote tumtegemee Mungu katika kila jambo, kwa kuomba na kushukuru. Tumsifu na kumuabudu Mungu Baba siku zote na wakati wote. Maana yeye ndiye yote katika wote.
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
Wakolosai 4:2
huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
1 Petro 5:7
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Wafilipi 4:7
Comments
Post a Comment