JE, WANAONYA KUNDI KUHUSU HATARI INAYOKUJA?
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike 5:3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ndugu, sisi tumekuwa wana wa nuru, wana wa mchana, sisi si wa usiku, wala wa giza hata siku ile itupate kama mwivi.
Tujivike vifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
Yeremia 6:14
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Mathayo 24:38-39
Comments
Post a Comment