KATIKA KUJENGA TABIA NJEMA, NINI KINGINE NI MUHIMU?
Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,
ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.
Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
Yuda 1:17-21
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kujijenga katika tabia njema ni kwa kuzidi katika kuomba na kujilinda na upendo wa Mungu kwetu kwa kuyakumbuka na kuyaishi mafundisho yaliyonenwa na mitume wa Kristo Yesu kuwa makini na watu wasio wa Roho , watu wa dunia hii tuu.
Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye, wenye kujengwa katika yeye, mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa na mkazidi kutoa shukrani.
Comments
Post a Comment