KIUHALISIA, NI IPI HALI YA WATU WOTE?
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Warumi 3:23
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kiuhalisia wote tumekuwa na dhambi, wa si kwa Wayahudi na Wayunani bali kwa wote walio chini ya sheria, chini ya torati. Dhambi huja kwa njia ya sheria, bali haki ya Mungu ipo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.
Warumi 3:24-25
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Warumi 5:1
Comments
Post a Comment