KRISTO ANALO JINA ASILOLIJUA MTU.
Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
Ufunuo wa Yohana 3:12
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Ufunuo wa Yohana 14:1
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kuna jina jipya la Kristo asilolijua mtu, ila litakuwa limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
1 Yohana 5:8
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 1:14
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
Ufunuo wa Yohana 19:16
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ufunuo wa Yohana 19:12-13
Hivyo, jina lake aitwa " NENO LA MUNGU".
Comments
Post a Comment