KWA NINI MAUTI HAIKUMSHIKILIA KRISTO KATIKA UTAWALA WAKE?
Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
1 Petro 2:22
Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
Yohana 8:46
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yesu hakutenda dhambi kabisa, ndicho kilichomuwezesha kuishinda mauti. Mauti haikuweza kumshikilia kwenye utawala wake yule mwovu. Pamoja na mateso yote, matukano na aibu zote, yeye alijikabidhi kwa Mungu ahukumuye kwa haki. Pamoja na yote hayo, alikuwa na uwezo wa kukataa, na kuuondoa mwenyewe uhai wake na kuutwaa tena.
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Isaya 53:7
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
1 Petro 2:23
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
Yohana 10:17
Hivyo, tunakiri Yesu ni Bwana, na twaamini Kristo alikufa na baada ya siku tatu akafufuka katika wafu.
Comments
Post a Comment