KWA NINI MUNGU ALIMTOA MWANAE MPENDWA AFE? NI NANI PEKEE ANAYEFAIDIKA NA KIFO CHAKE?
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Yohana 3:16-36
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Mungu aliupenda ulimwengu, ikiwa na maana aliwapenda watu wake wote, na alimtoa Mwanae kwa ajili ya wote. Nia ikiwa ni kila mmoja apate ule uzima wa milele aliotuandalia tokea mwanzo. Agizo ili kuupata uzima huo ni kumwamini Mwana aliyatumwa na yeye.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
1 Yohana 4:16
Hivyo, tunakiri Yesu ni Bwana, na twaamini Kristo alikufa na baada ya siku tatu akafufuka katika wafu ili kuupata uzima wa milele.
MUNGU ANATUPENDA, ANAPENDA WATU WAKE WOTE, NA SISI TUPENDANE.
Comments
Post a Comment