MWENYE MATUMAINI YA KUMUONA MUNGU HUFANYAJE?
Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tumeitwa Wana Wa Mungu na ndivyo tulivyo, na ulimwengu haututambui, na itakavyodhihirika, tutafanana naye, maana tutamwona kama alivyo tutakapouvua huu mwili wa kuharibika.
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
1 Yohana 3:1-2
Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
1 Yohana 3:4,7
Hivyo, tutende haki, kama yeye alivyo na haki. Tupendane sisi kwa sisi kama Kristo Yesu alivyotupa amri. Asiyependa hukaa katika mauti. Asiyetenda haki hatokani na Mungu, ni wa ibilisi.
Comments
Post a Comment