NI AHADI GANI KUBWA NA ZA THAMANI ZIMEAHIDIWA WASHINDI?
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
2 Petro 1:4
Ahimidiwe Mungu baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na baba yetu. Kwa kumjua Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo tumeahidiwa ahadi kubwa na za thamani. Na mojawapo ya ahadi kuu ni uzima wa milele.
Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Petro 1:2
Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.
1 Yohana 2:25
Hivyo, tumjue sana Mungu na kumkiri Yesu ndiye Kristo ili tupate hizo ahadi tulizoahidiwa kama washindi.
Comments
Post a Comment