NI LINI MAISHA HAYA YA UZIMA YATAWEKWA?
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
1 Wakorintho 15:51-52
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Sio wote tutalala, lakini wote tutabadilika siku ya parapanda ya mwisho,wafu watafufuliwa kwanza, wasiwe na uharibifu, na walio hai watabadilika.
"Miili hii ya kuharibika itavaa kutokuharibika na ya kufa itavaa kutokufa."
Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
1 Wakorintho 15:53
Hivyo, wapendwa tuimarike, tuzidi kutenda kazi ya Bwana siku zote, maana taabu sio bure katika Bwana.
Comments
Post a Comment