TUNAWEZAJE KUTOFAUTISHA KATI YA KWELI NA YA UWONGO?
Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi.
Bali ninyi mmegeuka mkaiacha njia; mmewakwaza watu wengi katika sheria; mmeliharibu agano la Lawi, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 2:7-8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yapasa midomo ya kuhani kunena yaliyo maarifa, yaliyo mema ili watu waifuate sheria kinywani mwake, maana yeye ni mjumbe wa Bwana. Kuhani inapoiacha njia sahihi anawakwaza watu wengi katika sheria.
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
Isaya 8:20
Sheria ya kweli ilikuwa kinywani mwake, wala udhalimu haukuonekana midomoni mwake; alikwenda pamoja nami katika amani na unyofu, na kuwageuza wengi hata wakaacha uovu.
Malaki 2:6
Comments
Post a Comment