UFUFUO WA KRISTO UMEKUWA FAIDA GANI KWETU?
Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.
1 Wakorintho 15:20
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa kufufuka Kristo katika wafu, kiyama ya wafu ipo, maana yeye ndiye limbuko lao. Na kama Kristo hakufufuka, imani yetu ni bure. Hivyo waliolala katika Kristo watahuishwa atakapokuja, na hapo ndio mwisho, Kristo atakapompa Mungu Baba ufalme wake.
Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
1 Wakorintho 15:21-22
Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
Warumi 5:18
Hivyo, tunakiri Yesu ni Bwana, na twaamini Kristo alikufa na baada ya siku tatu akafufuka katika wafu ili kuupata uzima wa milele.
Comments
Post a Comment