AGANO JIPYA LINASEMAJE KUHUSU KINYONGO?
Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Yakobo 5:9
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wengi wetu tumekuwa tukijifanya tunajua kusamehe kwa kusema " Nisamehe kabisa, lakini sitasahau". Hii ni kushikilia kinyongo. Tuangalie, tusije hukumiwa kwa kujidanganya huku.
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6:12,14,15
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Waefeso 4:32
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Wakolosai 3:13
Comments
Post a Comment