FANYENI YOTE KWA MOYO, MKIMSHUKURU MUNGU.
Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Wakolosai 3:24
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Unapofanya jambo, fanya kwa upendo ukijua kabisa unafanya kwa ajili ya Mungu wala si kwa wanadamu. Ukihudumu, ukiomba, ukitoa, na yote fanya kwa moyo ukijua unamtumikia Bwana na utapokea ujira kwa Bwana.
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
1 Petro 2:2
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Wakolosai 3:17
Comments
Post a Comment