HUU MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA MUNGU UMESABABISHA NINI TANGU NYAKATI ZA PAULO?
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
2 Wathesalonike 2:7-12
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana atakuja huyo ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu na ataketi katika hekalu la Mungu akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndiye Mungu.
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:3-4
Comments
Post a Comment