JE, BWANA ANASEMA NINI KUHUSU WACHUNGAJI WA UWONGO?
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Yeremia 50:6
Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?
Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo.
Ezekieli 34:2-3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Watu kwa kukosa maarifa ya Neno la Mungu mioyoni mwao wanaangamizwa , wanatangatanga kama kondoo aliyekosa mchungaji. Mtumwa wa Bwana asiwe mgomvi bali mwanana kwa watu wote, aweze kufundisha na awe mvumilivu. Watu wanachukia mema, wanapenda mabaya. Watamwomba Bwana, asiwaitikie, atawaficha uso wake wakati huo wa hukumu, kwa kadri walivyotenda mabaya kwa matendo yao.
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
1 Petro 5:2-3
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Luka 15:4
Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia.
Ezekieli 34:11
Comments
Post a Comment