JE, MUNGU HAKUKATAZA KINYONGO TANGU ZAMANI?
Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.
Mambo ya Walawi 19:18
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Usiwachukie wengine moyoni mwako, wala usichukue dhambi kwa ajili yao. Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
Warumi 12:17
Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Mathayo 5:48
Comments
Post a Comment