JE, NI MAELEZO YA KWELI KWAMBA AGANO JIPYA LILIFICHWA KWENYE LA KALE, NA AGANO LA KALE LIMEFUNULIWA KWENYE JIPYA?
JE, NI MAELEZO YA KWELI KWAMBA AGANO JIPYA LILIFICHWA KWENYE LA KALE, NA AGANO LA KALE LIMEFUNULIWA KWENYE JIPYA?
Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?
Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
Matendo ya Mitume 8:30-31
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ni ukweli kabisa Agano la Jipya lilifichwa kwenye la Kale, na Agano la Kale limefunuliwa kwenye Jipya. Ni kwa uwazi kabisa unaoonekana, Kristo amejulikana katika maandiko ya Agano la Kale. Bila Agano la Kale habari za Kristo kuwa ndiye Masihi zisingeimarika. Tusingependa kujifunza Biblia yote, kama Wayahudi, tungepoteza muelekeo wa vitu muhimu sana vilivyomo kwenye Agano Jipya lenyewe.
Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
Matendo ya Mitume 8:34-35
Comments
Post a Comment