JE, NI NINI MTU ANAHITAJI ILI AISHI
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Mathayo 4:4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Mtu anatakiwa apate chakula cha mwili na pia anatakiwa sana apate Neno La Mungu kama chakula cha kiroho ili aishi. Kama mtu anaishi kwa Neno la Mungu, anapaswa lazima kulitumia kila siku kwani ni lishe ya kila siku inayohitajika kumweka hai.
Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
Matendo ya Mitume 17:11
Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
Kumbukumbu la Torati 8:3
Comments
Post a Comment